STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya ameibuka na kufunua siri yake ambayo hajawahi kuisema kwamba, alipokuwa akisoma sekondari katika Shule ya St.Thomas alikuwa akivaa sketi ndefu mpaka chini kitendo kilichosababisha wanafunzi wenziye wampe jina la sista. Akizungumza na Ijumaa Wikienda Uwoya alisema alipokuwa ameanza kidato cha kwanza alikuwa mpole sana, wazazi wake wakamshonea sketi za shule ndefu mpaka mguuni kiasi ambacho

wenziye walikuwa wakimtania na kumuita sista na kwa wakati huo alikuwa akiona kawaida tu. “Yaani huwezi amini mtu akiniletea zile sketi leo naweza nisimuelewe kabisa na nitamshangaa sana, lakini mimi nilikuwa nazivaa wenzangu wananitania na kuniita Sista Irene,” alisema Uwoya.