Imam mkuu nchini Ghana ni mtu wa maneno machache lakini kiongozi huyo wa dini mwenye umri wa miaka 100 ana uwezo wa kuwaleta watu pamoja. Aliamua kusherehekia siku yake ya kuzaliwa kwa kuhudhuria misa ya kanisa katoliki.Sheikh Osman Sharubutu (C), in green, sitting in a pew at the Christ the King Catholic Church in Accra, Ghana

Picha za Sheikh Osman Sharubutu, akiwa ameketi katikati ya waumini wa Kikristo katika kanisa katoliki la Christ the King Catholic mjini Accra wakati wa ibada ya pasaka imezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Mufti huyo mkuu wa Ghana anawaakilisha waumini wa dini ya Kiislamu waliyo wachache, anataka kuhakikisha ameacha utawala wa amani katika uongozi wake – kama sehemu ya kuleta jamii pamoja bila kujali misingi yao ya kidini.

Mufti huyo mkuu wa Ghana anawaakilisha waumini wa dini ya Kiislamu waliyo wachache, anataka kuhakikisha ameacha utawala wa amani katika uongozi wake – kama sehemu ya kuleta jamii pamoja bila kujali misingi yao ya kidini

Hatua yake ya kuingia kanisani ilishabihiana na kisa cha makanisa kushambuliwa kwa mabomu na watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa Kiislam nchini Sri Lanka, ambapo watu zaidi ya 250 waliuawa makanisani na katika Hoteli za kifahari.

Wale wanaounga mkono hatua ya imam huyo walimtaja kama nuru inayoangaza gizani.Sio kila mtu aliyefurahishwa na hatua ya Sheikh Osman Sharubutu – wengine walisema ni laana, kwa muislamu kushiriki sala ya kikristo.

Lakini Sheikh Sharubutu anasisitiza kuwa hakuwa anashiriki maombi bali hatua yake ilikuwa ya kuimarisha uhusiano kati ya Waislamu na Wakriristo.

“Kiongozi huyu anajaribu kubadilisha dhana potovu kuhusiana na dini ya Kiislamu, kwamba ni dini inayochukia dini zingine,” msemaji wake Aremeyao Shaibu aliiambia BBC.