Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewaongoza Makamishna na Maofisa Wakuu Waandamiazi wa Jeshi hilo katika zoezi la usajili wa line za simu kwa kutumia alama za vidole linaloendeshwa kupitia makampuni mbalimbali ya simu za mkononi.

Akizungumza kabla ya kufanyika kwa zoezi hilo, IGP Simon Sirro amesema kuwa, zoezi la usajili kwa alama za vidole litasaidia katika kubaini uhalifu na wahalifu na kwamba hakuna mtu atakayeweza kujificha ili asibanwe na mkono wa sheria pale anapojihusisha na uhalifu ukiwemo wa kimtandao.

Aidha, IGP Sirro ameendelea kuwaonya wafanyakazi wa makampuni ya simu kuwa waaminifu wakati wanapotekeleza majukumu yao ili kujiepusha kujiingiza kwenye matukio ya kihalifu.