Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa chama wa Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole, ameteuliwa na waziri wa Ardhi William Lukuvi, kuwa mjumbe wa shirika la nyumba la taifa (NHC).

Waziri Lukuvi ameteua wajumbe hao 7 wa bodi ya shirika la nyumba la taifa, leo Mei 20, 2019 siku chache baada ya Rais Magufuli kumteua Dr. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa bodi hiyo.

Wajumbe walioteuliwa ni,

1. Bi. Immaculate Senye
2. Bi. Sauda Msemu
3. Bw. Abdallah Mwinyimvua
4. Bw. Humphrey Polepole
5. Bw. Martine Madeke
6. Eng. Mwita Rubirya
7. Bw. Charles Singili