Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema watu wanapaswa kujua ugumu wa kuwa na wadhifa huo na kuwataka wajifunze kuchuja baadhi ya maneno yanayowekwa katika mitandao ya kijamii kwa sababu mengi si ya kweli.

Ameyasema hayo katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Amesema wakati watu wakisema katika mitandao ya kijamii ni lazima wajue kazi ngumu aliyonayo.“Nafikiri baba Askofu (Dk Fredrick Shoo- mkuu wa KKKT) umeona ugumu wa kuwa spika, umejaribu tu kidogo umeona wewe mwenyewe shughuli iliyotokea.”

“Kwa hiyo mnaposema kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Ndugai mjue kazi ngumu niliyonayo,” alisema Ndugai.