Msanii wa Muziki, Jux amethibitisha kuwa amefikia hatua kubwa ya kukamilisha albamu yake ya kwanza ‘The Love Album’.

Kupitia Insta Story, Jux akiwa Studio alisema albamu hiyo imefikia asilimia 75 na itatoka hivi karibuni.

Mbali na kolabo zake na wasanii kutoka Tanzania, Wasanii 6 wa kimataifa wanatarajiwa kusikika kwenye album hiyo.

Kwa mujibu wa Jux, albamu hiyo inaweza kuwa na idadi ya nyimbo 14 baada ya kuchagua kutoka kwenye nyimbo Zaidi ya 40 ambazo asharekodi