Director Hanscana ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa kufanya kazi na mastaa tofauti tofauti na ameelezea stori yake ya maisha akimtaja na mtu aliyemfanya kufikia kuitwa Hanscana.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Hanscana amemtaja mwimbaji Mtanzania anaeishi Afrika Kusini Royazdad  na kusema kuwa ndie amemfungulia dunia ya kuwa Director na anaheshimu mchango wake kwenye maisha yake na aliongezea kuwa ni Msanii pekee ambaye alikubali kufanya nae kazi bila malipo yoyote.

“UTU NI HADHINA Nilikutana na @royazdad miaka 7 iliopita, nilikuwa naona talent ndani yangu lakini sijawahi shoot video hata moja ya kuangalia tu je talent ipoo au najipa tu moyo, Kukutana na huyu jamaa sjui ikawaje akatokea kutuamini mimi na @khalfani_khalmandro akasema ntawapa ngoma yangu moja mshoot lakini inabidi tushoot kesho maana keshokutwa me nasafiri naenda South Africa kutafuta maisha so nambieni nini niandae”

“Tukampa mahitaji yetu then jamaa akaandaa then akatuuliza HOW MUCH mnahitaji kufanya hii kazi? Nikamwambia just elfu arobaini tu ( 18$ ) nikakodi kamera na reflector, jamaa ananipa Elfu 60 ( 28$ ) ndo kwa mara ya kwanza mtu ananipa hela nikashoot video hapo mjue,Okay Next morning tukaanza kazi na tukafanikiwa kumaliza salama”“Then akanambia mimi from kesho ntakuwa sipatikani hewani mpaka mambo yangu yatapokuwa sawa huko SA kwahiyo ukimaliza ku edit wewe release tu then itavyokuwa tutajuwa juu kwa juu,Kweli next day jamaa akaelekea SA alipofika mpakani Tunduma akanicheki tena kuwa hatopatikana tena mpaka atapokuwa Okay so me nipambane na video coz ikionekana na mimi ndo ntapoonekana”

“Story ni ndefu ukurasa ni mdogoBut miaka mitatu tokea hapo ndo nikawa sasa HANSCANA huyu ninae post hapa mda huu na yeye akiwa @royazdad ,Jamaa kwa kifupi alinifungulia DUNIA yangu ya kuwa DIRECTOR naheshimu sana mchango wake kwangu na ndo msanii pekee ninashoot videos zake bila kumcharge anything anytime anywhere”