Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri Mji wa Mafinga wakijadili hoja za CAG
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe akizungumza wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri Mji wa Mafinga wakijadili hoja za CAG
NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.

MKUU wa mkoa wa Iringa, Ally Hapi ameiagiza Halmashauri ya Mji Mafinga kuhakikisha wanatenga na kuchangia asilimia 10 ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Wanawake ,Vijana na watu wenye Ulemamavu.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje wakati wa kikao maalum cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 37A(1) cha Sheria ya Fedha za Serika|i za Mitaa (marekebisho 2018) sura ya 290, suala la kuchangia asi|imia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kukopesha vikundi vya Wanawake, vijana na Watu wenye ulemavu vilivyosajiliwa ni la Kisheria kuanzia Julai, 2018.

Alisema kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Mwaka 2017/2018, inaonesha kuwa, Halmashauri ya Mji Mafinga ilichangia kwenye Mfuko huo ,kiasi cha shilingi milioni 90,000,000 tu badala ya shilingi 250,088,994 zilizopaswa kutolewa kutokana na kiasi cha shilingi 2,500,889,940 zilizokusanywa kama mapato ya ndani ya Halmashauri. Hivyo, halmashauri ilishindwa kuchangia shilingi 160,088,994 katika Mfuko wa Wanawake na Vijana

Kambelenje alisema kuwa matumaini serikali kwa halmashauri hiyo ni kutumia ushirikiano mzuri uliopo kuhakikisha kuwa, hoja zote za ukaguzi zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na zile za Mkaguzi ndani, zinashughulikiwa ipasavyo, ili ziweze kuhakikiwa na kufungwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo ya Serikali.

“Naamini kuwa, mafanikio haya mazuri yametokana na uwepo wa ushirikiano Mzuri baina yenu Waheshimiwa Madiwani, Watendaji na Wadau mbalimbali wa Halmashauri. Wito wangu kwenu ni kuwa, muendelee kudumisha ushirikiano huu, ili Halmashauri iendelee kupata Hati Safi katika kaguzi zote kila mwaka na pia kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga.”

Alisema kuwa licha ya hoja ya kutenga fedha kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu kwa mujibu wa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizoishia tarehe 30 Juni, 2018, Halmashauri ya mji Mafinga ina jumla ya hoja 38 ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi.

Aidha alitoa wito kwa Halmashauri iweze kuwa na mifumo bora na imara udhibiti wa ndani, itakayosaidia kulinda na kusimamia ipasav matumizi sahihi ya rasilimali na mapato ya Halmashauri, naiagi Halmashauri ihakikishe kuwa, inakiimarisha kitengo chake Ukaguzi wa ndani kwa kukiwezesha kuwa na wataalam ‘ kutosha na vitendea kazi vya kutosha, ili kiweze kutekele majukumu yake ipasavyo kwa wakati na ukamilifu unaostahili.

Aliitaka halmashauri ihakikishe kuwa, inasimamia mali zote kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali iliyopo ikiwa kwa kwa mujibu wa agizo la 45(1) la Memoranda ya Fedha za Serikali la Mitaa ya Mwaka 2009 ambayo inaeleza kuwa kuwa, Mali zote ambazo hazitumiki hususan zilizochakaa zitambuliwe na kuwasilishwa kwenye Kamati ya Fedha pamoja na Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupata idhini ya kutumwa Wizara ya Fedha ili kuundiwa Bodi ya kuvikagua kwa hatua ya kuvifuta na kuviondosha kama kanuni ya 254 ya kanuni za fedha za mwaka 2001 inavyoelekeza.

Kambelenje aliongeza kuwa halmashauri ihakikishe kuwa, inaweka utaratibu wa kulipa madeni yanayofikia kiasi cha shilingi milioni 510,042,225 ambayo yametokana na madai ya wakandarasi, watoa huduma mbalimbali na watumishi kama ilivyobainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya mwaka 2017/2018. 

“Naagiza kuwa, madeni yote yanayostahili kulipwa na fedha za makusanyo ya ndani yahakikiwe na yalipwe mara moja na yale yanayostahili kulipwa na Serikali Kuu, Halmashauri ifanye ufuatiliaji kuhakikisha fedha hizo zinatolewa na kulipwa”” alisema

Aidha, alitoa wito kwa Halmashauri kuacha kulimbikiza au kuongeza madeni hivyo ni vema malipo ya huduma zinazotolewa kwenye Halmashauri ihakikishe kuwa fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo zinatumika baada ya kupata idhini ya kamati ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo.

Akizungumzia hoja hizo makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe alisema kuwa watahakikisha hoja zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni ambayo halmashauri inadaiwa.