Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe anapiga mnada mali zake kadhaa ikiwemo matrekta makubwa na ya kisasa matano na zana nyengine za kilimo.

Tangazo lililotolewa na kampuni ya kunadisha mali, linaonesha kuwa Bw Mugabe amepanga kuuza magari yapatayo 40, ikiwemo gari moja la kifahari na magari matano aina ya Toyota Hilux pick-up.

Mugabe aling'olewa madarakani na jeshi mwaka 2017.

Wachambuzi wanaamini hatua hiyo ya kuuza mali inaweza kuashiria kuwa biashara ya familia ya Mugabe - ambayo inamiliki mashamba makubwa 21 - inaweza ikawa inapitia wakati mgumu kifedha.

Mkoba uliojaa madola ya Mugabe waibiwa
Rais wa zamani Robert Mugabe 'hawezi kutembea'
Mambo tisa ambayo huyajui kuhusu Mugabe
Mnada huo unatarajiwa kufanyika leo Jumamosi na kuongozwa na kampuni ya Ruby Auctions katika shamba lake lake la Gushungo.

Shamba hilo lipo katika eneo maarufu na la kifahari, na ndani yake kuna jumba la makazi la kifahari pia.