Ikiwa ni siku mbili zimepita toka chama cha soka nchini Italia (FIGC) kitangaze kuwa kimemfungia miezi mitatu kufanya shughuli za uwakali wa wachezaji nchini Italia Mino Raiola ambaye ni wakala wa wachezaji mbalimbali duniani akiwemo Paul Pogb wa Man United.

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA nalo limekazia adhabu hiyo na kutangaza kuwa Mino Raiola atatumikia adhabu hiyo duniani kote na sio Italia pekee, sababu sahihi za kwani nini Mino Raiola kafungiwa bado hazijawekwa wazi ila inatajwa kuwa inawezekana ni kauli yake aliyoitoa miezi kadhaa kuwa FIGC ni dhaifu na haoni ikikua.

Zlatan na Raiola
Kutokana na kupewa adhabu hiyo ambayo itamalizika hadi August 9 yaani siku moja baada ya dirisha la usajili la England kufungwa, hiyo itakuwa ni pigo kwa wateja wake kama Paul Pogba, Mario Balotelli, Lorenzo Insigne, Moise Kean, Henrikh Mkhitaryan na Matthijs de Ligt, Raiola kwa sasa anasimami wachezaji 20 katika bara la Ulaya.

Hata hivyo Raiola amewahi kuingia katika mvutano kukosolewa na watu mbalimbali kuhusiana na namna anavyofanya kazi yake ikiwemo Sir Alex Ferguson na kocha wa Juventus Massimiliano Allegri, binamu yake Mino Raiola anayefahamika kwa jina la Vincenzo amefungiwa kwa miezi miwili,  hivyo kufuatia adhabu hiyo wateja wake (Wachezaji) kama watataka kuhama majira ya joto watalazimka kuvunja mkatana na Raiola au wasubiri adhabu yake iishe.