Mwigizaji wa Bongo Movie, Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu 'Sugu', amefunguka kuwa ameamua kuacha kila kitu na kufanya yale ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Faiza amesema kuwa, kuna kipindi alikuwa yuko kwenye wakati mgumu lakini kwa nguvu za Mungu alitoka sehemu moja na kwenda nyingine hivyo lazima kurudisha utukufu kwake kwa kufanya atakayo.

“Kwa sasa nafunga kabisa kwa nia moja na kuacha kila kitu kinachoenda kinyume na Mwenyezi Mungu, nafunga na ni hivi sasa nimeokoka Kiislam maana wengine wanajua wokovu ni kwa Wakristo tu, lakini hata kwetu (kwenye Uislam) kuna kuokoka", amesema Faiza.

Mwanamama huyo mwenye watoto wawili alikuwa kwenye mgogoro na mzazi mwenzie Sugu ambaye ndiye baba wa mtoto wake wa kwanza aitwaye Sasha.

Baada ya wawili hao kutengana, Sugu aliweka wazi uhusiano wake mwingine, kitendo ambacho Faiza hakufurahishwa nacho na mara nyingi amekuwa akisema kuwa japo walitengana lakini anampenda baba huyo wa mtoto wake.