NDICHO kilichobaki tu! Mwigizaji wa filamu za Kibongo ambaye ni baby mama wa Mbunge wa Mbeya-Mjini, Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu, Faiza Ally ameamua kuacha kila kitu na kufanya yale ya kumpendeza Mwenyezi Mungu. Faiza ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, kuna kipindi alikuwa yuko kwenye wakati mgumu mno, lakini kwa nguvu za Mungu alitoka sehemu moja na kwenda nyingine hivyo lazima kurudisha utukufu kwake kwa kufanya atakayo.

“Kwa sasa nafunga kabisa kwa nia moja na kuacha kila kitu kinachoenda kinyume na Mwenyezi Mungu, nafunga na ni hivi sasa nimeokoka Kiislam maana wengine wanajua wokovu ni kwa Wakristo tu, lakini hata kwetu (kwenye Uislam) kuna kuokoka,” anasema Faiza ambaye ni mama wa watoto wawili.