WAKATI wengine wakisubiri penzi la Mbongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na mama mtoto wake Fahyma waachane, mambo yamekuwa tofauti kwani mrembo huyo amekiri kumpa mambo adimu jamaa huyo na kusema kwamba hata iweje hawezi kuachika.

Akipiga stori na SHUSHA PUMZI, Fahyma alisema, wanaotamani aachane na mzazi mwenzake wanapoteza muda, kwa vile hawawezi kuachana leo wala kesho kutokana na mapenzi ya dhati anayompata, hivyo ni bora wakafanya mambo mengine ya maana kuliko kuendelea kumtamani mwanaume wake.

“Unajua watu wengi hawapendi mapenzi yangu mimi na Rayvanny, yaani wanatamani hata kesho tuachane, lakini hicho kitu hakiwezekani kwa sababu mambo ninayompa tukiwa wawili sio rahisi kunisahau, kwa hiyo wanapoteza tu muda. Bora waendelee kufanya vitu vyao vya maana kuliko kufuatilia maisha yetu,” alisema.

STORI: Memorise Richard