Emirates Group leo imetangaza faida ikiwa ni mwaka wake wa 31 mfulululizo pamoja na ongezeko la biashara.

Hayo yametangazwa leo katika ripoti yake ya mwaka ya 2018-19. Emirates Group imepata faida ya AED 2.3 bilioni (US$ 631 milioni) kwa mwaka wa fedha ulioishia 31 Machi 2019, ambayo imepungua kwa silimia 44 ikilinganishwa na mwaka jana. Mapato ya kampuni yalifika AED 109.3 bilioni (US$ 29.8 bilioni), sawa na ongezeko la asilimia 7 ikilinganishwa na mwaka jana. Salio (cash balance) ilikuwa AED 22.2 bilioni (US$ 6.0 billion), ambayo ilipungua kwa asilimia 13 ikilinganishwa na mwaka jana kwa sababu ya uwekezaji mkubwa uliofanywa ambayo ni pamoja na ununuzi mkubwa na ulipaji wa gawio la mwaka jana lililofikia AED 2 bilioni (US$ 545 milioni).

Kutokana na faida yote, Emirates Group ilitangaza gawio la AED 500 milioni (US$ 136 milioni) kwa Shirika la Uwekezaji la Dubai. (Investment Corporation of Dubai) kwa mwaka 2018-19.

Mwenyekiti na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Emirates na Emirates Group, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum, alisema: “2018-19 umekuwa mwaka mgumu kwetu kwani hatukufanya vizuri sana kama tulivyotegemea. Ongezeko la bei ya mafuta na kuimarika kwa Dola ya Kimerekani kuliathiri mno mapato yetu, huku pia ushindani ukiongezeka katika masoko yetu makubwa. Kupungua kwa shughuli za anga duniani kote kuliathiri mapato ya dnata na Emirates kwa ujumla.

“Kila mzunguko wa biashara ni tofauti na tunaendelea kufanya kila jitihada kukabiliana na changamoto na pia kutumia vizuri fursa zinazokuja. Lengo letu siku zote ni kujenga biashara yenye faida, endelevu na yenye heshima Dubai na misingi hii inaendelea kutuongoza katika maamuzi na uwekezaji wetu.

Mwaka 2018-19, Emirates na dnata zilirekodi faida kwa mwaka wa 31 mfulululizo, ukuaji wa biashara na uwekezaji katika jitihada na miundombinu ambavyo vinatuhakikishia mafanikio ya baadaye.

Katika mwaka 2018-19, Emirates Group iliwekeza AED 14.6 bilioni (US$ 3.9 bilioni) katika ndege mpya , vifaa, ununuzi wa makampuni, mitambo ya kisasa, teknolojia ya kisasa, wafanyakazi, ambavyo vyote hivi vilisababisha ongezeko la matumizi kufikia AED 9.0 bilioni (US$ 2.5 bilioni).

Mwezi Februari, ilitangaza kuwa inakusudia kununua ndege aina ya A330-900s zipatazo 40 na A350-900s zipatazo 30 zenye thamani ya US$ 21.4 bilioni kulingana na makubaliano na Kampuni ya Airbus na ndege hizi zitawasilishwa kuanzia mwaka 2021 hadi 2024. Shirika hilo pia litapokea ndege 14 aina ya A380 kuanzia 2019 hadi 2021, hizvi kufanya oda nzima ya A380 kufikia 123.

Uwekezaji wa dnata’s katika waka huu ulihusisha ununuzi wa Q Catering na Snap Fresh huko Australia, na 121 Inflight Catering kule Marekani, ununuzi wa hisa na hivi kuwa mmiliki wa Dubai Express, Freightworks LLC; na ununuzi wa hisa asilimia 51 za BollorĂ© Logistics LLC, UAE; ujenzi wa vifaa vya kupakia na kupakua mizigo kule Ubelgiji, Marekani, Uingereza, Uholanzi, Australia, Singapore na Pakistan; Ununuzi wa Kampuni ya Kitalii huko Ujerumani iitwayo Tropo na hisa nyingi zaidi katika Kampuni ya BD4travel, ambayo inatoa taarifa mbalimbali za kimtandao katika sekta ya usafirishaji.

Katika makampuni yake zaidi ya 120, nguvu kazi ya Emirates Group iliongezeka kwa asilimia 2 na kufikia 105, 286 ambao wanawakilisha mataifa 160. Ongezeko hili linatokana na dnata kujitanua zaidi kimataifa.

Sheikh Ahmed alisema: “Katika mwaka 2018-19, tuliimarisha nidhamu katika matumizi huku tukitanua biashara na kuongeza mapato. Tumejitahidi kutowekeza sana katika masuala ambayo sio ya uendeshaji huku tukiwekeza katika teknolojia mpya zaidi na mifumo mipya ya kazi na hivi kuongeza uzalishaji.

Alimalizia: “Ni vigumu sana kutabiri mwaka unaokuja lakini Emirates na dnata ziko katika nafasi nzuri ya kukabiliana na changamoto ili kufanikiwa katika soko la dunia. Ni lazima tuendelee kuja mbinu mpya ikiwemo uwekezaji katika watu wetu, teknolojia na miundombinu ili kukabiliana na ushindani na kubakia kileleni. Kama kampuni inayojali tumewekeza pia katika kusaidia jamii mbalimbali, utunzaji wa mazingira na pia kukuza talanta na ubunifu ambavyo vitatusaidia kukua katika siku zijazo.

Utendaji wa Emirates

Abiria na mizigo iliyobebewa na Emirates ilifikia ATKM 63.3 bilioni kufikia mwishoni mwa mwaka 2018-19 na hivi kuifanya iendelee kuwa shirika kubwa ziadi la ndege kimataifa. Shirika hilo liliongeza uwezo wake kwa asilimia 3 ili kuongeza ufanisi.

Emirates ilipokea ndege mpya 13 katika mwaka huu wa fedha ambazo ni pamoja na A380s saba and Boeing 777-300ERs sita, ambazo ni pamoja na oda ya mwisho ya 777-300ER. Ndege aina ya 777 itawasilishwa mwaka 2020, wakati Emirates itapokea ndege yake ya kwanza ya 777X.

Katika mwaka 2018-19, Emirates iliondoa ndege 11 za zamani na hivi kubakiza ndege 270 hadi mwisho wa mwezi Machi. Zoezi hili lililohusisha ndege 24 ndio kubwa kuwahi kufanyika katika mwaka mmoja na hivi kufanya wastani wa umri wa ndege za Emirates kuwa miaka 6.1.

Hii inaifanya Emirates iweze kuendeleza mkakati wake wa kurusha ndege mpya zaidi na kutekeleza ahadi yake ijulikanayo kama ‘Safiri Vizuri Zaidi- Fly Better’ ambayo ni nzuri kwa mazingira, utendaji na pia kwa abiria.

Katika waka huu, Emirates ilianzisha safari tatu mpya ambazo ni pamoja na: London Stansted (UK), Santiago (Chile) na Edinburgh (Scotland), na pia kurudisha safari ya Sabiha Gokcen (Turkey). Pia iliongeza uwezo wa kubeba abiria zaidi na mizigo katika safari zake 14 na kupandisha hadhi ya safari katika miji sita huku wakiwapa wasafiri wigo mpana wa kuchagua muda wa kusafiri na kuunganisha safari.

Ili kuimarisha ukuaji wake duniani, Emirates ilisaini mikataba na Jetstar Pacific na China Southern Airlines. Pia imeboresha ubia wake wa kibiashara na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).

Ushirikiano kati ya Emirates na flydubai ulizidi kukua zaidi huku wateja wa Emirates sasa wakiweza kufika maeneo 67 zaidi ambayo yanahudumiwa na flydubai kwa kupitia ndege 11 zinazotumia temino No 3. Ushirikiano huu pia umeshuhudia Programu maalumu kwa wateja ijulikanayo kama Skywards ikitumiwa na Emirates na flydubai kwa pamoja.

Licha ya kuwepo na ushindani mkubwa katika masoko yake, Emirates imeongeza mapato yake kwa a silimia 6 hadi kufikia AED 97.9 bilioni (US$ 26.7 bilioni). Kuimarika kwa Dola ya Kimarekani kulikuwa na athari kubwa sana katika faida ya Emirates mwaka huu kwani faida ilishuka kutoka AED 661 milioni (US$ 180 milioni) mwaka uliopita na kufikia AED 572 milioni (US$ 156 milioni) mwaka huu wa fedha.

Gharama za uendeshaji ziliongezeka kwa asilimia 8 mwaka wa fedha 2017-18. Wastani wa bei ya mafuta ya ndege iliongezeka kwa asilimia 22 katika mwaka huu wa fedha baada ya ongezeka la asilimia 15. Kufuatia ongezeko la asilimia 3 katika uwezo wa wa ndege, gharama ya mafuta iliongezeka kwa asilimia 25 kwa mwaka jana na kufikia AED 30.8 bilioni (US$ 8.4 bilioni). Hii ndio gharama kubwa zaidi ya mafuta kwa Emirates kwa miaka yote na ni asilimia 32 ya gharama za uendeshaji ikilinganishwa na asilimia 28 katika mwaka wa 2017-18. Mafuta yameendelea kuwa na gharama kubwa zaidi katika uendeshaji wa shirika.

Licha ya changamoto zote hizi, Emirates bado iliweza kupata fadida ya AED 871 milioni (US$ 237 millioni), ambayo hata hivyo imeshuka kwa asilimia 69 decline of 69% ikilinganishwa na mwaka jana na hivi kuwelka pengo la asilimia 0.9 katika faida.

Idadi ya abiria ilizidi kuongezeka kwani kwa mwaka huu Emirates ilisafirisha abiria milioni 58.6 (ongezeko la asilimia 0.2). Idadi ya viti katika ndege iliongezeka kwa asilimia 4 huku shirika likihakikisha viti vimekaliwa kwa asilimia 76.8 ambayo ilipungua kutoka asilimia 77.5 mwaka uliopita na hii ilitokana na kudorora kwa uchumi ambao ulisababisha safari za angani kupungua na pia kulikuwa na ushindani mkubwa katika masoko mengi.

Katika mwaka huu, Emirates iliweza kutafuta kiasi cha fedha kipatacho AED 14.2 bilioni (US$ 3.9 bilioni) kwa kupitia mikopo, taasisi za fedha na ukodishaji

Ndege sita aina ya 777-300ER zilinunuliwa kwa kupitia utaratibu maalumu kutoka Japan ujulikanao ‘Japanese Operating Lease with a Call Option (JOLCO)’ ambapo kwa kupitia utaratibu huu, Emirates iliweza kukusanya zaidi ya AED 28 bilioni (US$ 7.6 bilioni) kutoka Japan tangu mwaka 2014.

Utaratibu mwingine ujulikano kama sukuk wenye thamani ya US$ 600 milioni ulitumika kununua ndege mbili aina ya A380 na ndege tano nyingine aina ya A380 zilinunuliwa kwa utaratibu wa mkpo kutoka kwa mashirika tofauti yaliyopo Korea, Ujerumani, Uingereza na Mashariki ya Kati.

Taratibu zote hizi za mikopo zinadhihirisha ni jinsi gani Emirates ina uwezo na inaaminika kama shirika kubwa la ndege duniani.

Emirates closed ilifunga mwaka huu wa fedha na rasilimali za fedha (cash assets) zipatazo AED 17.0 billion (US$ 4.6 bilioni).

Mapato kutoka maeneo yote sita ambayo Emirates ina uwakilishi yalikuwa na uwiano sawa na hakuna eneo ambalo lilitoa zaidi ya asilimia 30 ya mapato. Uropa iliongoza kwa AED 28.3 billion (US$ 7.7 billion), ambalo ni ongezeko la asilimia 6 kutoka 2017-18. Asia ya Mashariki na Australia zinafuatia kwa AED 26.6 billion (US$ 7.2 billion), ongezeko la 5%. Ukanda wa Marekani AED 14.5 billion (US$ 3.9 billion), ongezeko la 8%. Africa AED 10.2 billion (US$ 2.8 billion), ongezeko la 9%, Ukanada wa Guba na Mashariki ya Kati mapato yalipungua kwa asilimia 3 na kufikia AED 8.3 billion (US$ 2.3 billion). Katika Asia Magharibi na Bahari la Hindi mapato yaliongezeka kwa asilimia 6 na kufikia AED 8.1 billion (US$ 2.2 billion).

Katika mwaka huu wa fedha, Emirates ilifanya maboresho kadhaa kwenye bidhaa na huduma zake kwenye ndege na katika maeneo ya uendeshaji.

Dondoo: Ukamilishaji wa programu yenye thamani ya US$ 150 million kukarabati madaraja ya biashara na madaraja ya kawaida ya ndege zote za Boeing 77-200LR, ukarabati wa eneo lijulikanalo kama vintage ambalo lina mivinyo iliyotunzwa kwa zaidi ya miaka 15 na bidhaa mpya kabisa katika madaraja ya kwanza nay a biashara kwa kushirikiana na Bowers & Wilkins, Bulgari na BYREDO.

Emirates pia ilianzisha utaratibu ambao abiria sasa wanaweza kuhakiki safari zao (check in) wakiwa nyumbani , hotelini au ofisini na mizigo yao inaweza kusafirishwa kabla ya safari; iliongeza eneo maalumu la kusubiria (lounge) Cairo na kukarabati lounge za New York na Roma na pia kuzindua majaribio maalumu kwa marubani ‘biometric path’ katika Uwanja wa Ndege wa Dubai kwa kutumia teknolojia mpya kabisa ya bayometria ili kuwasaidia wasafiri wa Emirates wakati wanapohakiki safari zao (check in) wanapopita katika hatua ya uhamiaji na wakati wa kupanda ndege.

Kuhusu mtandao, Emirates imekuwa ya kwanza kuzindua viti vyenye muundo mpya wa 3D kwa kutumia teknolojia mpya ya mtandao ambapo pamoja na mambo mengine abiria wanaweza kuchagua bidhaa mbalimbali na huduma zinazopatikana katika ndege za Emirates ikiwemo sinema, mziki na burudani nyingine zilizopo na kuunganisha na vifaa vyao kama vile simu kabla ya safari.

Emirates SkyCargo iliendelea kufanya vizuri licha ya kuwepo na ushindani mkubwa na ilichangia asilimia 14 ya mapato ya Emirates.

Kitengo cha mizigo cha Emirates kiliingiza AED 13.1 billion (US$ 3.6 billion), sawa na ongezeko la 5% mwaka jana, wakati mizigo kwa ujazo wa tani uliongezeka kwa asilimia 1 kufikia tani milioni 2.

FTKM iliongezeka kwa mwaka wa ppili mfulululizo iliongezeka kwa asilimia 3 huku ikionesha uwezo mkubwa wa SkyCargo kuendelea kupata wateja wenye thamani kubwa licha ya bei ya mafuta kuongezeka na kudoroka kwa masoko mengi.

Ndege za mizigo zilizotumiwa na SkyCargo zilifikia 12 (Boeing 77F). SkyCargo ilianzisha huduma mpya ya mizigo kwenda Bogota (Colombia) na pia kurejesha huduma ya mizio iendayo Erbil (Iraq).

Emirates SkyCargo katika mwezi wa Aprili, ilizindua huduma mpya ya kusafirisha vifaa vya ndege kwa haraka kote duniani. MMwezi Agosti pia ilizindua huduma maalumu ya kusafirisha viatilifu na wanyama. Kuna pia huduma ya kuangalia wanyama, kushughulikia nyaraka zao wakati wa kusafirisha na kuwakatia tiketi za ndege za kurudi.

Hoteli za Emirates zilikusanya mapato yanayofikia AED 669 million (US$ 182 million), ambayo yameshuka kwa asilimia 10 mwaka uliopita huku ushundani ukiw amkubwa sana UAE.

Utendaji wa dnata

Kwa mwaka 2018-19, dnata ilipata faida kubwa sana katika miaka yote huku ikitengeneza faida ya AED 1.4 billion (US$ 394 million). Hii ni pamoja na uuzaji wa hisa zake zipatazo asilimia 22 katika kampuni ya Hogg Robinson Group (HRG), ambayo ilinunuliwa na Amex Travel Business Group. Bila kufanya biashara hii ya kuuza hisa, faida ingekuwa chini kwa asilimia 15 ikilinganishwa na muda kama huo mwaka jana.

Mapato ya dnata yaliongeza hadi AED 14.4 billion (US$ 3.9 billion), ongezeko la 10%. Hii inadhihirisha ukuaji wa kampuni hii katika maeneo yake yote. Biashara ya kimataigfa ya dnata inatoa asilimia 70 ya mapato ya dnata.

Dnata imewekeza takriban AED 1.1 billion (US$ 314 million) makampuni mengine, vifaa vipya, teknolojia na watu katika mwaka huu.

Katika mwaka 2018-19 gharama za uendeshaji za dnata ziliongezeka kwa asilimia 11 na kufikia AED 13.1 billion (US$ 3.6 billion).

Salio la dnata’s (cash balance) lilikuwa AED 5.1 billion (US$ 1.4 billion), sawa n aongezeko la asilimia 4. Kampuni hiyo ilitoa AED 1.4 billion (US$ 386 million) ikiwa ni fedha za uendeshaji mwaka 2018-19 ambazo ziliendana na uhalisia na hivi kuifanya kampuni hiyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuwezesha kufadhili uwekezaji wake.

Mapato kutoka shughuli za dnata katika Uwanja wa Ndege wa UAE ziliongezeka kwa asilimia 2 na kufikia AED 3.2 billion (US$ 878 million).

Idadi ya ndege zilizohudumiwa na dnate UAE ni 211,000. Hii inaonesha athari za changamoto zilizopokatika sekta ya anga katika ukanda huu na jinsi zinavyoathiri wateja wa dnata. Biashara ya mizigo inayoshugulikiwa na dnata ilikuwa kwa asilimia 1 hadi tani 727,000 ambayo ilisababishwa na kuporomoka kwa soko la mizigo.

Katika mwaka wa 2018-19, dnata iliimarisha biashara yake ya mizigo kwa kununua hisa zaidi na ikawa mmiliki pekee wa Dubai Express na Freightworks LLC; na hisa 51% na hivi kuwa mwanahisa mkuu wa Bolloré Logistics LLC, UAE ambayoo inafanya kazi katika nchi 106.

dnata pia ilinunua hisa nyingi zaidi katika kampuni ya DUBZ, kampuni ambayo ilitokana nan a programu maalumu iitwayo Intelak, inayotoa huduma ya kuwasilisha mabegi kwa wasafiri wanaowasili Dubai na kwa abiria wanaosafiri kuelekea Dubai kupata pasii za kupanda ndege kutoka sehemu yoyote Jijini.

Iliwekeza katika teknolojia na uendeshaji na pia namna ya kumridhisha mteja. Baadhi ya mambo yaliyofanywa ni uzinduzi wa kituo cha usimamizi wa rasilimali, kifaa kipya katika eneo la mizigo ili kuhakikisha zoezi zima linarahisishwa.

Shughuli za dnata katika uwanja wa ndege zilishuhudia mapato yake yakikuwa kwa asilimia 5 na kufikia AED 4.0 billion (US$ 1.1 billion), kwa kuongeza biashara, kufungua maeneo mapya na kusaini mikataba mipya. Shughuli katika viwanja vya ndege vya kimataifa zinaendelea kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa dnata. Ndege zilizohudumiwa na kampuni hiyo ziliongezeka kwa asilimia 9 kufikia 488,000 na mizigi pia iliongezeka kwa asilimia 1 kufikia tani milioni 2.4.

Katika mwaka huu, dnata ilishinda mikataba mipya zaidi ya 100 katika masoko makubwa ambayo ni pamoja na Marekani, Canada, Uingereza, Australia, Italia.

dnata pia iliongeza uwezo wake wa kuhudumia mizigo katika mwaka 2018-19. Iliimarisha shughuli zake kule Ubelgiji kwa kuzindua kituo cha mizigo chenye ukubwa wa 14,000 m² katika Uwanja wa Ndege wa Brussels na pia kuimarisha shughuli zake za mizigo huko Dallas, London Heathrow, Adelaide na Karachi na pia kufanya ukarabati huko Singapore na Amsterdam. Kuhusu ukuaji wa wateja, dnata iliwekeza katika upanuzi wa Gatwick na Manchester na kufungua huduma mpya ya mizigo katika viwanja vya ndege vya Islamabad na Multanna pia kule Pakistan ambapo wamefunga mitambo ya kisasa ya mizigo.

dnata iliwekeza katika mitambo ya pharma na hivi kuwa kampuni yenye uwezo kuliko zote kuhudumia mizigo kule Uingereza, Uholanzi, Australia na UK, the Netherlands, Australia na Singapore. Uwezo huu umetambuliwa na IATA kule Dubai, na Tromto na pia kutambuliwa na GDP huko London na Zurich.

Huko Italia, dnata iliongeza hisa zake na kufikia asilimia 70 katika kampuni ya SpA ambayo inatoa huduma zake kule Milan. Dnata ilipewa leseni ya kufanya shughuli zake katika Uwanja wa Ndege wa Zurich hadi mwaka 2025 increased its share in Airport Handling SpA, a Milan-based ground handler, to 70%. Huko Amerika ya Kaskazini, dnata ilizindua shughuli zake katika Uwanja wa ndege wa Los Angeles na kuanza kutoa huduma kwa wateja katika Uwanja wa Ndege wa JFK ulioko New York.

Biashara ya dnata ya chakula zillingizia dnata AED 2.6 billion (US$ 717 million) ambayo ni ongezeko la asilimia 23. Dnata ilisambaza zaidi ya milo milioni 70 kwa wateja wa ndege ikiwa ni ongezeko la asilimia 27.

Mafanikio haya yalisababishwa pamoja na mambo mengine uwekezaji katika Qantas’ catering, Q Catering na Snap Fresh huko Australia, na 121 Inflight Catering huko Marekani na pia kuingia katika ubia mbalimbali hasa kule UAE, Romania, Jamhuri ya Czech na Italia.

Katika mwaka huo dnata ilizindua sehemu ya kuandaa chakula ya kisasa yenye ukubwa wa 2,000 m² na yenye uwezo wa kuandaa milo 60,000 kwa mwezi huko Canberra.

Huko Amerika ya Kaskazini, dnata ilizindua shughuli zake huko New York, Nashville na Orlando kwa kuinunua 121 Inflight Catering na inatarajia kuanza huko Boston, Houston na Vancouver katika robo ya kwanza ya mwaka ujao wa kifedha huku miradi mingine ikitajajiwa katika maeneo mengine ya Marekani.

Mapato kutoka huduma za usafirishaji za dnata yameongezeka kwa asilimia 9 hadi AED 3.7 billion (US$ 1.0 billion). Mapato ya huduma zote za usafirishaji zilikuwa AED 11.5 billion (US$ 3.1 billion).

Hii inaonesha jinsi gani dnata imeweza kupenya katika soko hasa katika masoko yake ya Uingereza na UAE ambayo imekuwa ikisuasua licha ya kuwa masoko makubwa.

Mwaka 2018-19, dnata ilipenya katika soko la Ujerumani na kuongeza wigo wake wa usafirishaji huko Uropa huku ikinunua Tropo, ambayo ni kampuni ya kitalii inayofanya biashara kwa njia ya mtandao na pia kwa kutumia mawakala. Ilinunua pia hisa katika BD4travel (Big Data for Travel), kampuni ambayo inajihusisha na masuala ya kiintelijensia katika sekta ua usafiri kwa kupitia mtandao.

dnata pia iliimarisha kituo chake cha mawsiliano kwa kukamilisha mradi wake wa pili huko Belgrade huku ikiwa na maeneo 14 inamofanya kazi huko UAE, Serbia, Ufilipino, India na Uingereza. Kampuni hiyo pia imejiimarisha kwa lusaini mkataba wa miaka 5 na Shirika la Ngdege la Etihad kuhudumia vituo vyake vya mawasiliano duniani.

Ripoti nzima ya mwaka 2018-19 ya Emirates Group –Emirates, dnata na makampuni yake mengine inapatikana: https://www.emirates.com/ae/english/about-us/business-model/financial-transparency.aspx

1US$ ni sawa na 3.67AED