RAPA kutoka  Canada, Drake,  ameamua kuionyesha ndee yake binafsi (private jet) kupitia ukurasa wake wa Instagram.  Ndege hiyo iliyopewa jina la ‘Air Drake’,  thamani yake haijajulikana.


Ndege hiyo binafsi imekuja kutokana na dili ambalo Drake alisaini na kampuni ya Cargo Jet, ambapo kampuni hiyo ya ndege ina makazi yake nchini Canada. Inaripotiwa kuwa mmiliki wa Cargo Jet, Ajay Virmani, ameingia makubaliano ya kibiashara na Drake, hivyo kutengenezewa ndege hiyo inayotajwa kuwa ni moja ya makubaliano ya mkataba wao.
Drake anatajwa kuwa ni miongoni mwa mastaa wenye pesa nyingi Marekani ambapo  aliwahi kununua nyumba yenye thamani ya Tsh Bilioni 6 za Tanzania  ambapo pia inaelezwa kuwa  anamiliki nyumba tatu zilizomgharimu zaidi Sh. Bilioni 10 za Tanzania.