MSANII wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ amesema baada ya kuachana na staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya hategemei tena kutoka kimapenzi na staa yeyote.

Dogo Janja aliyazungumza hayo leo katika mahojiano na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio ambapo alisema kuwa, ameuchezea sana utoto na kwa sasa ni muda wa kupumzika.

“Sitaki kudate ‘kutoka kimapenzi’ na mwanamke ambaye ni maarufu. Kwa sababu nimeshauchezea utoto wangu vizuri na ujana wangu pia. Ni raha sana ukiona mtoto anacheza na mtu mzima lakini ni vibaya ukiona mtu mzima anacheza na mtoto.

“Kingine unajua kuna watu wengine hawajacheza utotoni kwa hiyo wanaona ni kipindi cha kuchezea utoto wao,” alisema Dogo Janja.