Taasisi ya Doris Mollel (DMF) kwa kushirikiana na Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA) wametoa wa chakula kwa wananchi wasiojiweza katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia muendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambao unaelekea ukingozi sasa. msaada huo ulihusisha Mchele, Mafuta, tende nk.

Wakati huohuo, Ubalozi wa Oman nchini ulishirikiana na Taasisi ya Doris Mollel katika kuwazawadia mavazi wananchi hao kwa maandalizi wa sikukuu ya Eid el Fitr, ambapo walipatia Kanzu, Vikoi na Khanga kwa wakina mama. msaada huo umegusa kaya 250 za vijiji mbalimbali vya wilaya ya Bagamoyo ikiwemo Kitopeni, Mataya, Buma Madrasa, Ramiya na Makurunge. Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alishirikiana na Taasisi ya Doris Mollel katika kulifanikisha zoezi hilo kikamilifu. Zoezi hilo limefanyika jana Mei 28, 2019.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF), Rahma Amood (wa pili kushoto) kwa pamoja na Mratibu wa Shughuli za Kijamii wa Taasisi hiyo, Maryam Gerion wakikabidhi sehemu ya msaada kwa wakazi wa Kijiji cha Mataya, wilayani Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia muendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, vilivyotolewa kwa ushirikiano na Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA), jana Mei 28, 2019.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) amshukuru Mratibu Msaidizi wa Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA), Ali Ozkaya kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kufanikisha zoezi hilo kwa wananchi wa Bagamoyo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF), Rahma Amood.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akishikiana na Afisa kutoka TIKA, Ibrahim Mohamed kutoa msaada wa chakula kwa wananchi wa kijiji cha Kitopeni, wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood na Mratibu wa Shughuli za Kijamii wa Taasisi hiyo, Maryam Gerion wakikabidhi sehemu ya msaada kwa wakazi wa Kijiji cha Buma, wilayani Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia muendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, vilivyotolewa kwa ushirikiano na Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA), jana Mei 28, 2019.