Msanii mkongwe kwenye filamu za kibongo, Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’ ameeleza kuwa kwa sasa ameamua kuiweka pembeni sanaa na kujikita zaidi kwenye shughuli zake za U-mc.

Dk Cheni amesema kutokana na hali ya soko la sanaa ilivyo ameamua kujikita katika shughuli zake za sherehe kwa maana ya kupiga muziki, MC na kupiga picha kwani kwake ameona zinamuingizia kipato tofauti na uigizaji.

“Acha niusome kwanza mchezo kwa upande huu, sijaitupa sanaa moja kwa moja ipo siku mashabiki wanaweza kuniona kwenye gemu kama kawaida soko litakapokaa vizuri,” alisema Dk Cheni