Mwongozaji maarufu wa video za wasanii wa Bongo Fleva, Director Ivan anadaiwa kula pesa ya msanii chipukizi, Mr. Kesho na kushindwa kufanya video yake.


Akizungumzia tuhuma hizo katika Friday Night Live (FNL) ya EATV, Mr. Kesho amesema kuwa kitendo alichofanya Director Ivan kwake ni dharau kubwa na kama angekuwa ni mtu mwenye hasira wangepigana.

“Ivan amenidharau sana na kama angekuwa mtu mwingine mwenye roho mbaya angempiga au kumfanyia kitu chochote. Nilimpa pesa na nilitakiwa kushoot nyimbo yangu na Shilole”, amesema Mr. Kesho.

“Nilimpa Sh 300,000 na iPhone 6 plus, yenye thamani ya laki 7  ambayo nilikuwa natumia mimi mwenyewe, nakumbuka aliniambia tutashoot tukaenda Bagamoyo lakini akaniweka kwenye ratiba moja na mtu wa Singeli, yaani akaniunganisha. Tulishoot kipande kimoja tuu akasema tutaendelea siku nyingine ikawa basi”, ameongeza.

Director Ivan amekuwa kwenye malumbano kadhaa na baaadhi ya wasanii, huku wengi wakilalamika kuwa hawakamilishiwi kazi zao kwa wakati.

Mtazame hapa msanii huyo akieleza alivyopoteza pesa yake kwa Director Ivan.