Dereva wa basi la Abood lenye namba za usajili T 269 DBV ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kifo kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira baada ya kugonga pikipiki aina ya Boxer. 

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbezi Kwa Msuguri baada ya gari hilo lililokuwa linafukuzana na basi lingine la BM katika barabara mpya na kuigknga pikipiki.

Baada ya tukio hilo dereva wa Abood alishuka kwa lengo la kuangalia kilichotokea, ndipo wananchi walipomvamia na kuanza kumshambulia, kabla ya kufanikiwa kuiombia na kurudi kwenye gari na kujifungia milango.
Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa abiria ambao walikuwa wakitaharuki na kulazikika kutokea madirishani mpaka hapo walipofika polisi na kumuamuru dereva kufungua milango la kutoka nje.

Hakuna aliyefariki katika ajali hiyo, huku abiria wa bodaboda (jina lake halikufahamika) alijeruhiwa kwenye mguu, kichwani na mkononi na amekimbizwa katika hospitaki ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguri.