DC Akanusha Mtu Kujinyonga Bali Alinyongwa
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole amethibitisha Mkazi wa kijiji cha Nyakahako Kata Chifunfu Wilaya Sengerema mkoani Mwanza Tumaini Faustine (35) aliyeripotiwa kuwa amejinyonga  alinyongwa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutelekezwa juu ya mti.

Kipole alisema kuwa kifo cha kijana huyo kinazua utata kwa kuwa alikutwa na majeraha shingoni huku Kichwani akiwa amepigwa na kitu chenye nchi kali pamoja na damu kutoka masikioni suala lililozua utata mkubwa

Kipole alieleza kuwa siyo kawaida kwa mtu aliyejinyonga kumkuta anajeraha shingoni kichwani huku akivuja damu masikioni dalili hizo zinadhihilisha wazi kuwa alinyongwa kisha mwili wake kutundikwa juu ya mti.

"Jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi juu tukio hilo ili kuwabaini watu walihusika kwenye tukio hilo na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaobainika," alisema Kipole.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Kituo cha Afya ya Ngomamtimba kilichoko Kata ya Chifunfu John Ishengoma alisema baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi ulikutwa na majeraha shingoni, kichwani kama kapigwa na kitu chenye nchi kali pamoja na kutokwa damu masikioni na kuzua utata juu ya kujinyonga kwake.

Afisa Mtendaji Kata ya Chifunfu Kibasa Masangwa alisema marehemu huyo alizikwa  kijijini kwako Nyakahako Kata ya Chifunfu.

Aidha Baba wa kijana huyo ambaye ni marehemu Mzee Imani Faustine alisema kijana wake alitoweka siku tatu zilizopita nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha na hapakuwa na ugomvi wa aina yoyote na kusikitishwa na tukio la mwanaye kujingonga