Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akibandika moja ya magari ambayo yaliletwa kwenye usajili ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika kituo cha Chuo Kikuu Ardhi nyenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal. Anayeshuhudia ni dereva wa gari hilo.
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo kwa dereva mara baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo cheti cha utambuzi kwa kwa dereva mara baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam.
Magari yakipata yakijaziwa maji tayari kwenda kuuza. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) limeanza kutekeleza zoezi la usajili na utoaji wa vibali kwa magari ya kusambaza majisafi (water Bowsers) katika jiji la Dar es Salaam na Pwani.
Zoezi hilo la Usajili litaendeshwa kwa wiki mbili kuanzia Mei 15 litadumu kwa wiki mbili mpaka Mei 29, 2019 eneo la kituo cha Chuo Kikuu Ardhi nyenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal, Tegeta na Bagamoyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akisimamia zoezi hilo Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi amesema kuwa zoezi hilo linalengo la kuwatambua wauzaji wote wa majisafi ikiwa na kuangalia usalama wa vyombo wanavyotumia kuwauzia maji wananchi.
"Niwaombe wote wenye kufanyabiashara ya majisafi kujitokeza ili tuweze kuwatambua na kuwapa leseni na kuwapa mikakati yenye lengo la kujenga ili watoe huduma salama," amesema Mkonyi.
Zoezi hilo la usajili linamtaka mwenye gari kuja na vielelezo ikiwemo picha moja ya rangi ya mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA au HATI YA KUSAFIRIA).
Kingine ni Nakala ya kasi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya dereva vyote viwe vimethibitishwa na mwanasheria.
Amesema kuwa matenki yatakayokuwa yamekidhi vigezo vya kupata usajili yatasafishwa na dawa maalumu ya kuua wadudu kwenye mantenki na kubandikwa stika ya DAWASA.
Amesisitiza kuwa baada ya zoezi hilo kuisha Mei 29, 2019 gari litakalokuwa halijasajiliwa halitaruhusiwa kuendesha biashara ya kutoa huduma ya kuuza maji na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwa endapo watayaona magari hayo yakitoa huduma bila kuwa na vibali ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.