MZAZI mwenziye na muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’, Chuchu Hans amesema kuwa mpaka sasa watu wengi wako kwenye sintofahamu juu ya penzi lake na mzazi mwenzie huyo kama wameachana au la; na yeye anapenda iwe hivyo.  Akizungumza na Amani, Chuchu alisema kuwa watu wengi wanadhani kuwa walishaachana na kila mtu yuko na mambo yake lakini wanashangazwa zaidi wanapomuona anatoka nyumbani kwa Ray.

“Unajua watu wengi wako kwenye fumbo kuhusu mimi na Ray, na mimi nataka wawe hivyohivyo kwani sio kila kitu chetu kiwepo wazi kwa kila mtu ukizingatia sisi ni wazazi,” alisema Chuchu. Chuchu na Ray walidaiwa kumwagana miezi kadhaa iliyopita huku mapichapicha ya Ray akiwa na mwanamke mpya yakizagaa mitandaoni ambapo mwenyewe alipoulizwa alikanusha kuwa huyo anayeonekana naye si mpenzi wake.