Leo May 28,2019 inaelezwa kuwa mkali wa RnB Chris Brown ameitwa nchini Ufaransa kwa ajili ya kukutana na msichana ambaye alimtuhumu kwa ubakaji mapema mwaka huu kati ya tarehe January 15- 16 kwenye hoteli ya Le Mandarin Oriental.

Inaripotiwa kuwa kikao hicho tayari kimeandaliwa kufanyika kwenye Makao Makuu ya polisi Paris siku ya Jumanne tarehe 4,June, pia kwa upande wa msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 inadaiwa kuwa May 26 aliwasilisha ushahidi wake na hivyo kilichobaki ni mahudhurio ya mkali huyo wa RnB.

January 22,2019 Chris Brown alishikiliwa na polisi kwa tuhuma hizo za ubakaji na kuwekwa rumande, saa 24 na baadae aliachiwa huru na kurudi Marekani na pia aliwahi kukanusha taarifa hizo na kusema kuwa zilikua zikimchafua.