Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Prof.Mussa Assad amesema maeneo yote ya umma yanayofanyiwa ukaguzi ni lazima kutoa ushirikiano hasa kwenye kujibu hoja na mapendekezo ya kikaguzi ili kuiwezesha ofisi yake kufanya kazi kwa wakati.

Utakumbuka April 10, 2019, Prof. Assad aliwasilisha Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Taarifa za Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.

Pia siku hiyo hiyo, ripoti za CAG ziliwasilishwa Bungeni baada ya vuta ni kuvute, hatua hiyo imeondoa wingu jeusi lililokuwa linazagaa kwa wiki kadhaa juu ya utata wa kikatiba kuhusiana ushirikiano wa Bunge na CAG.

Ni baada ya Bunge kupitisha azimio la kutofanya kazi na Prof. Assad kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Bunge ni dhaifu