USHINDI walioupata Simba leo mbele ya Sindida United kwa kuifunga mabao 2-0 uwanja wa Namfua umetosha kutetea ubingwa wao walioutwaa msimu uliopita.

Mabao mawili  ya Simba yaliyopachikwa na Meddie Kagere dakika ya 9 na John Bocco dakika ya 60 yametosha kuwapa ubingwa.

 Simba imecheza jumla ya michezo 36 na imefikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi msimu huu, ikiwa bado na michezo miwili kibindoni.

Huu ni ubingwa wa pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita 2017/18 ikiwa njiani kuelekea Singida, na ni ubingwa wake wa 20 kwenye ligi hiyo, nyuma ya mabingwa wa kihistoria, Yanga ambao wameshachukua ubingwa huo mara 27.

Michezo iliyobaki kwa Simba ni kati ya Biashara United na Mtibwa Sugar ambapo mchezo mmoja dhidi ya Biashara Unite watakuwa Uhuru na ule wa Mtibwa Sugar watakuwa Morogoro uwanja wa Jamhuri.

Ushindi huo utafanya warejee tena kwenye michuano ya kimataifa ambapo msimu huu walifika hatua ya robo fainali.