Boeing 737 Max Itachukua Muda Kurejea Angani
Shirika la Kimataifa linalohusika na safari za anga IATA linataraji kwamba itachukua muda wa hadi mwezi Agosti mpaka ndege aina ya Boeing 737 Max zinatakapoanza tena kufanya kazi. 

Mkuu wa shirika hilo ametoa taarifa hiyo leo akiongeza kusema kwamba uamuzi wa mwisho kuhusu suala hilo utatolewa na wasimamizi wa kampuni hiyo. Ndege za Boeing 737 Max zilizuiwa kuruka duniani mwezi Machi baada ya kutokea ajali mbaya nchini Ethiopia iliyouwa watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, ambapo ilikuwa ni ajali ya pili kubwa katika kipindi cha miezi mitano kusababishwa na aina hiyo ya ndege ya Boeing.