Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Sugu amebahatika kupata mtoto wa kiume na ameamua kumpa jina la Shawn Joseph Mbilinyi na kueleza sababu za kumuita mwanaye ‘Shawn’ .


Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Rapper huyo mkongwe nchini Tanzania, amesema kuwa amempa jina la Shawn kwani lina maana ya ‘ZAWADI TOKA KWA MUNGU’ ndio maana akachagua jina hilo.

Kwa upande mwingine, amesema jina hilo amekopi kwa rapper Jay-Z ambaye jina lake halisi ni Shawn Carter na kueleza gwiji huyo wa muziki ana Falsafa za kutokata tamaa na ni mtafutaji pia.

“Pia ni katika kumuenzi Msanii na Mfanyabiashara maarufu duniani JAY-Z, ambaye jina lake halisi ni SHAWN CARTER… Hii ni kutokana na jinsi FALSAFA zake kuhusu HUSTLING zilivyonisaidia kufika hapa nilipo kwenye maisha.. Asanteni sana,” ameandika Sugu kwenye ukurasa wake wa Instagram.