Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Moise Katumbi Chapwe, amerejea nyumbani mjini Lubumbashi nchini baada ya kuishi uhamishoni nchini Ubelgiji, amepokelewa na maelfu ya wafuasi wake.

Katumbi amekuwa akiishi nje ya nchi hiyo kwa karibu miaka mitatu, baada ya kukimbilia nje ya nchi kwa sababu ya tofauti za kisiasa na Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila.
Akiwa Ubelgiji Katumbi alifunguliwa mashtaka ya kuuza nyumba ambayo sio ya kwake na akahukumiwa jela miaka mitatu, lakini baadaye mashataka hayo yakafutwa.

Mwaka 2018, alijaribu kurejea nyumbani kuwania Urais lakini akazuiwa na Maafisa wa usalama alipofika katika mpaka wa Kasumbalesha, upande wa Zambia.