Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amesema ushindi walioupata jana wa goli 3-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar yalikuwa ndio malengo yao makubwa.

Magoli ya jana ya Simba SC yalifungwa na Nahodha wao John Bocco,  Clatous Chama na Emamanuel Okwi.

"Tulitawala mchezo, tulitengeneza nafasi na tulifanikiwa kufunga. Jambo muhimu tumekaribia lengo letu." alisema Kocha Patrick Aussems.

Kwa matokeo ya jana Simba SC iliweza kurejea kwenye usukani wa Ligi kwa kufikisha pointi 85 walizojikusanyia katika michezo 34 waliocheza, wakiwa wamebakiza michezo minne.