Beki wa Ndanda FC, Abdallah Mfuko amefunguka baada ya kupata kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba SC na kusema kuwa walishindwa kuwadhibiti Simba kutokana na ubora wao pamoja na wao kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.

"Haikuwa bahati yetu, tulipambana kutafuta matokeo tukakwama, ila ukweli ni kwamba Simba ipo vizuri na ndio maana tukapoteza.

"Tumetengeneza nafasi lakini zote ziliweza kuzuiwa na wapinzani wetu, bado tunaendelea na mapambano kwa ajili ya michezo yetu iliyobaki muda bado unaruhusu makosa yetu benchi limeyaona na linafanyia kazi," amesema