Msanii wa Filamu, Shamsa Ford amewashauri watu maarufu wajitokeze kwa wingi kupima VVU hadharani ili kuwahamasisha vijana wengi kujitokeza kupima afya zao.

Shamsa kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa ana mshukuru Mwenyezi Mungu kwa ujasiri aliompa kuweza kupima afya.

"Kwanza kabisaa Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa ujasiri alionipa wa kuweza kupima afya yangu huku mamia ya watu wakinishuhudia.Ningeomba pia watu maarufu wajitokeze kwa wingi kupima hadharani ili kuwahamasisha vijana wengi kujitokeza kupima afya zao," aliandika Shamsa.

"Vijana wenzangu linapokuja suala la kujenga taifa haijalishi una maambukizi au huna tunapaswa kushikamana na kulijenga taifa.Wewe kijana uliyejifungia ndani na kukatisha ndoto yako kisa umepima umekutwa umeathirika toka nje itafute ndoto yako kuwa muathirika si mwisho wa maisha."

"Naongea na wewe mama uliyekata tamaa ya kufanya kazi kisa una maambukizi huku watoto wamekuzunguka wanakutegemea toka nje fanya kazi si mwisho wa maisha..Usimnyoshee kidole mwenzio bali tuthaminiane na tupeane moyo pamoja tunaweza."

Siku chache zilizopita, Ilidaiwa Shamsa na mume wake, Chiddi Mapenzi wameachana.