Wakati msimu wa Ligi Kuu Bara ukielekea ukingoni, matajiri wa jiji la Dar es Salaam Azam FC wameanza harakati za kumnyakua kipa Beno Kakolanya.

Azam wametajwa kuanza mazungumzo na kipa huyo ambaye amekuwa hana timu kwa takribani nusu ya msimu mzima.

Kakolanya ni kipa huru hivi sasa baada ya iliyokuwa timu yake ya Yanga kuvunja rasmi mkataba wake.

Mchezaji huyo alitemwa kikosini na Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kufuatia kujiondoa ndani ya timu akidai stahki zake.

Kakolanya aliamua kufanya maamuzi hayo mazito baada ya kushindwa kuvumilia namna stahiki zake hizo zilivyochelewa kwa yeye kupatiwa.