STAA wa filamu Aunt Ezekiel, amefunguka kuwa wiki yote amekuwa na majonzi makubwa kutokana na kumkumbuka sana marehemu mama yake kitu ambacho kilimfanya kujifungia ndani na kulia.

Akizungumza na Za Motomoto, Aunt alisema kuwa ingawaje kampoteza mama yake muda mrefu lakini kuna kipindi anakaa na kumkumbuka sana huku akitamani hata dakika chache cha kuzungumza naye.

“Unajua kuna kipindi unakutana nacho unatamani mtu wa kuzungumza naye lakini ndani ya moyo unaona mtu wa kumueleza ya moyoni ni mama yako na yeye hayupo wala huwezi kumuona,” alisema Aunt kwa uchungu.