UNAWEZA kusikia kitu ukajenga maswali mengi kichwani imekuwaje kikatokea! Polisi wa eneo la Brayan West Campus, Nebraska mjini Lincoln, Uingereza wanamshikilia njemba mmoja, Peter Jacobsson kwa kosa la kufyatua bastola katika sehemu zake za siri.

Polisi wanasema kuwa, Peter, 32, alikuwa eneo hilo kwa upande wa kituo cha basi ambapo bastola ilikuwa ndani ya mfuko wake wa suruali na baada ya muda aliifyatuka na kupiga sehemu zake za siri.

Hata hivyo, Peter alikimbizwa katika Hospitali ya Irvingdale mjini hapo akiwa chini ya ulinzi wa polisi. Hata hivyo haijafahamika hasa sababu ya kujifyatua risasi.

Mmoja wa maofisa wa polisi kutoka Kituo Kikuu cha Lincoln, Luke Bonkiewicz alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:45 usiku ambapo walimkuta Peter akiwa hoi baada ya kufyatua risasi mfukoni kwake.