MWANAMUZIKI maarufu wa Bongo Fleva, Amini Mwinyimkuu ameamua kufunguka kuwa, anatamani sana kuzaa na mwanamuziki mwenzake Esterlina Sanga ‘Linah’, ambaye kwa sasa ni mpenzi wake ambapo huko nyuma walishawahi kuwa wapenzi wakamwagana kisha kurudiana. Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Amini alisema kuwa kama kuna kitu ambacho anakitamani zaidi mwaka huu ni kumpachika mpenzi wake huyo mimba ili tu roho yake itulie kitu ambacho anakiomba sana kwa Mungu, kitokee na anaamini kwa mapenzi yake kitatimia.
“Hakuna mtu ambaye anajua kilichopo moyoni mwangu, nia yangu kubwa ni kuzaa na Linah, napenda kuwa na mtoto naye si unajua kama mwanamke unayempenda unatamani kuzaa naye ndio ilivyo kwa Linah, na Mungu akipenda ni mwaka huu mambo yatakuwa mazuri,” alisema Amini ambaye leo anatarajia kuachia video ya wimbo wao mpya waliofanya na Linah unaokwenda kwa jina la Nimenasa.
Wawili hao kabla ya kurudiana hivi karibuni na penzi lao la sasa kuwa motomoto, waliwahi kuachana miaka kadhaa iliyopita na kila mtu akashika hamsini zake kwa kuwa na mtu mwingine. Baada ya kila mmoja kumwagana na mtuwe kwa nyakati tofauti, wameamua kurejesha penzi lao kwa kasi na sasa wamekuwa wakigandana kama ilivyokuwa zamani wakati penzi lao linachipukia