Baada ya Zest kusema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii na wa muziki wa Bongo fleva Amber Lulu, Msanii huyo amesema anashangaa sana kumuona Zest akizungumza maneno kama hayo wakati yeye anamchukulia kama kaka yake.Amber Lulu ameaiambia eNewz kuwa hawezi kuongea baya lolote kwa Zest kwa kuwa yeye anamchukulia kama ndugu ambao wametoka wote mkoa mmoja Mbeya, na ni mtu ambaye alichangia pia katika mafanikio aliyonayo katika fani yake ya muziki kwani alihusika sana kwenye wimbo wake wa Jini Kisirani.

"Kitu pekee ambacho nataka kumwambia Zest ni kwamba mimi bado namuheshimu kama kaka na siwezi kumtolea 'shit' kwa kuwa namuheshimu hivyo namuomba na yeye aniheshimu kwa maana hata mimi hawezi kuwa aina ya wanaume ninaowapenda na sijui kwanini kaongea alichoongea mimi sioni haja ya kumjibu namuacha aongee anachojisikia kuongea ili aridhishe nafsi yake". aliongea Amber Lulu.

Akimalizia Amber Lulu hakusita kutoa tahadhari kwa waandaaji wa wimbo wake wa sasa na kusema  kuwa anatoa wimbo mwingine mkubwa kushinda Jini Kisirani hivyo anawaomba wasije wakawa na roho za kukunja nyimbo hizo zitakapokuwa hit.