Kufuatia wito wa Spika wa Bunge,Job Ndugai juu ya kumtaka Mwakilishi wa Tanzania katika bunge la Afrika ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Bunge hilo Stephen Masele kurudi nchini mara moja,Mbunge huyo amesema kuwa hawezi kuzungumzia chochote juu ya yaliyokea Tanzania na kusema kuwa wakati ukifika atazunguzma na vyombo kueleza hali halisi.

Aidha Masele amesema hana taarifa rasmi iliyomfikia kutoka kwa Spika Ndugai inayomtaka kurudi nchini zaidi ya kusoma taarifa hizo kwenye Vyombo vya habari.

Hapo jana Spika Ndugai amesema kuwa amemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi wa Stehen Masele hadi Kamati ya Maadili itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

"Katika uwakilishi wa Bunge la Afrika kumetokea matatizo makubwa hasa kwa Mhe.Steven Masele matatizo ya kinidhamu,Tumelazimika kumrudisha nyumbani kuanzia Jumatatu, badala yake amekuwa akionyesha kugoma, ni kiongozi ambaye anafanya mambo ya hovyo hovyo" alieleza Spika Ndugai.