KAJALASTAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kutoa neno kwa mastaa wenzake kuhusiana na mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ambapo amewaasa kufanya matendo mema.

Akizungumza na mwandishi wetu, Kajala alisema kuwa anatamani kuona mastaa wote wakionyesha ukarimu na kujihifadhi kwa mavazi ya staha ili kuupa heshima mwezi huu wa Ramadhani.

“Najua wengine ni madhehebu tofauti kama mimi, lakini kikubwa siku zote ni kuheshimu kile wenzetu wanakiheshimu kwa sababu ni muda wa mwezi mmoja, hivyo inapendeza kila mtu akasimama kwenye maadili,” alisema Kajala.