Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Masanja Mkandamizaji amefunguka baada ya video iliyosambaa siku za hivi karibuni ikidaiwa kuwa ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Masanja amesema kuwa Polisi wakishafanya uchunguzi tutajua na atakuwa na kitu cha kuzungumza huku akisema kuwa ile video kwa mujibu wa maelezo ya mhusika alisema imetengenezwa kwahiyo tusubiri uchunguzi.

"Yah nina lolote kwasababu ishu iko Polisi na wanafanya uchunguzi tutajua baada ya uchunguzi kumalizika from there tutakuwa na kitu cha kuzungumza ," alisema Masanja.

"So Far sio kweli ile picha inayoonekana pale sio yeye inaonekana imetengezwa kwa mujibu maelezo yaliyopo kwahiyo tunasubiri tuone na uchunguzi utakavyofanyika tuone ni nani."