Msemaji wa Simba SC, Haji Manara ameonyesha furaha yake mara baada ya timu yake kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) 2018/19.

Haji amewapongeza wachezaji wa kikosi hicho kwa kazi kubwa waliyofanya kwa msimu mzima pamoja na benchi la ufundi.

"Tuwapongeze sana Wachezaji wetu wote, Benchi la ufundi chini ya Chief coach Patrick Aussems,lakini kipekee tuwashukuru nyie Wanachama na Washabiki wetu ambao ninaamini ndio chachu ya huu ubingwa. Always kwangu Star wa kwanza Simba ni Mshabiki wetu,Thanks a lot Guys," ameeleza Haji.

Utakumbika Simba SC wamenyakua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2018/19 baada ya kuichapa Singida United mabao 2-0 kwenye uwanja wa Namfua Singida.

Kwenye ushindi huo magoli ya Simba yamefungwa na Meddie Kagere dakika ya 10, na John Bocco 60. Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi msimu huu, ikiwa bado ina michezo miwili mkononi.