Mwanafunzi wa shule ya msingi Silver Mjini Babati Mkoani Manyara, Osiligi Paul mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita amefariki dunia baada ya kutokea ajali mbaya.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara, Augostino Senga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha basi la kampuni ya Mtei kugongana na basi dogo aina ya Hiace eneo la Himiti mjini Babati.