Msanii wa bongo fleva Amber Lulu amefunguka na kudai hayamsumbui maneno anayotupiwa na watu mitandaoni kwa yeye kupiga picha za nusu uchi kwa kuwa mtu pekee anayemuhofia ambaye ni Baba yake hayupo katika mitandao hiyo ya kijamii.
 

Amber Lulu ameeleza baada ya kuandamwa kwa kipindi kirefu akiwa na watu kuhusu kupiga picha akiwa mtupu na kuweka katika mitandao ya kijamii jambo ambalo lilisababisha baadhi ya watu kudhani mrembo huyo pengine hana wazazi ndiyo maana anajitoa akili kwa kupiga picha za aina hizo.
 

"Dingi nashukuru Mungu siyo mtu wa kufuatilia sana mitandao ya kijamii hasa Instagram 'maybe' aone gazeti na kwenye we abahatishe sana, siyo mtu mfuatiliaji. Kwa hiyo vitu vingi vinakuwa vinapita havijui", alisema Amber Lulu.
 

Pamoja na hayo Amber Lulu aliendelea kwa kusema "Baba yangu anafahamu ninapokaa, siyo kwamba nimetoka huko sijaaga. Niko vizuri yaani nimetoka huko nilipokuwa na baraka zote ndiyo maana naweza kufanya kitu na Mungu naye akaweka baraka zake na nikaweza kum-move on hizo zote ni baraka zake"