ALI KIBA AVUTWA SEHEMU NYETI NA MZUNGU LAIVU


Staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
Mwanamuziki anayefanya poa kuliko wasanii wote wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ amekuwa habari kufuatia Mzungu mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja kumvuta sehemu zake nyeti alipokuwa kwenye shoo pande za Marekani.

Kiba ambaye amekuwa akifanya shoo kibao ndani na nje ya Bongo, alikutana na kimbwanga hicho, mwishoni mwa wiki iliyopita alipokwenda kupafomu katika tamasha lililofahamika kwa jina la One Africa Music Festival.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Kiba alikutana na kisanga hicho mara baada ya kukamua ngoma zake kali zikiwemo Chekecha Cheketua na Mwana na alipokuwa anashuka, Mzungu huyo akamvaa na kumshika sehemu nyeti.

“Yule Mzungu nafikiri alikuwa amezidisha ‘mambo’ sasa Kiba wakati anashuka tu, akamdandia na kumshika maeneo nyeti. Ila uzuri ni kwamba mabaunsa waliwahi na kumtoa,” kilidai chanzo.
Chanzo hicho kilieleza kuwa, Kiba hakukasirishwa na kitendo hicho kwani alielewa kabisa Mzungu huyo ameguswa sana na muziki wake kwani hata alipokuwa anamfuata, alionekana kuimba Wimbo wa Aje kabla ya kumkumbatia na kumshika sehemu hizo nyeti.

“Kiba alibaki anacheka tu. Alienda zake moja kwa moja kupumzika katika hoteli aliyofikia na kuacha huko nyuma watu wakiendelea kumjadili Mzungu huyo,” kilizidi kueleza chanzo.
Ijumaa lilimvutia waya Kiba lakini ili kumsikia anazungumziaje tukio hilo lakini simu yake haikuwa hewani.
Hata hivyo, Ijumaa lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa mameneja wa msanii huyo ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai lilikuwa la kawaida hivyo kwa kuwa si la kikazi, asingependa atambulishwe kwa jina.

“Si unajua tena mashabiki huwa wanakunywa vitu vikali sasa yule dada wa Kizungu inaonekana alivutiwa sana na nyimbo za Kiba ila alipomkumbatia ndio yakatokea hayo.
“Ilikuwa ni ndani ya sekunde kadhaa tu lakini mabaunsa walimtoa fasta yule dada na Kiba alibaki anacheka tu ila hiyo nimekupa tu usinitaje maana si suala la kikazi,” alisema meneja huyo.