Wananchi Waliopo Dar es Saalam Kupatiwa Matibabu Bure

Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Saalam iliyo chini ya mheshimiwa Paul Makonda imeratibu tukio maalum litakalofanyika siku ya tarehe 24-25/09/2015 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Ambapo wananchi watakaojitokeza kwenye tukio hilo maalum watapatiwa matibabu bure.
Taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa kupitia akaunti yake ya Instagram imeeleza kwamba wananchi watapata fursa ya kupimwa magonjwa zaidi ya kumi (10) na kupatiwa matibabu bure.

Hivyo wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi.