Mr Blue: Ubishoo Kwenye Muziki Niliuanzisha Mimi
Mr Blue

Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amesema yeye ana mchango mkubwa katika mabadiliko ya muziki wa bongofleva nchini.
Akiongea katika kipindi cha Ndoto Kubwa cha Clouds TV Jumapili hii, Mr Blue amesema yeye ndiye msanii wa kwanza kufanya muziki akiwa na swagga.


“Mimi baada ya kuingia kwenye muziki kuna vitu ambavyo nilivifanya mimi kama mimi ili kuonyesha utofauti, kuanzia kwenye kuvaa, swagga za kuimba, kutoboa masikio. Kwa hiyo hivyo vyote kwa wakati ule watu walikuwa wananiona huyu jamaa vipi, kumbe mimi tayari nilikuwa nimeshaiona future, ndio maana wasanii wengi waofanya muziki kwa swagga, utasikia ana flow kama Mr Blue, tayari tulishaacha alama huko ndiyo maana tunaendelea kufanishwa,”

Katika hatua nyingine Blue amesema yeye alikuwa anapenda kusoma kuliko kufanya muziki, lakini akaamua kujifunza kufanya muziki mpaka akaweza.