Jokate Mwegelo amesisitiza kauli yake aliyoitoa kwenye Instagram mwezi uliopita kuwa anatamani kuona Alikiba na Diamond siku moja wanafanya collabo.
Akiongea kwenye kipindi cha 5 Select cha EATV hivi karibuni, Jokate alidai kuwa ili collabo hiyo iwe nzuri, ni muhimu iwe halisi na wala isilazimishwe.

Pia alidai kuwa haoni sababu tena ya kujenga bifu na ex wake Diamond kwakuwa ameshakua kiumri na kwamba ni muhimu kushirikiana ili kuonesha ushawishi wao.

Hata hivyo Jokate aliendelea kusisitiza kuwa yeye na Alikiba ni marafiki tu na kukanusha kuwa na uhusiano.
“We are just friends, we are better than that,” alisema.