DIAMOND ANUNUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI MOJA YA KITANZANIA

Huenda Diamond Platnumz akawa ameitimiza ndoto aliyokuwa nayo kwa miaka mingi – kumiliki gari alipendalo zaidi, Rolls Royce.
DIAMOND ANUNUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI MOJA YA KITANZANIA
Kwa muda mrefu, staa huyo amekuwa akisema kuwa hilo ndilo gari analotaka kulimiki kiasi cha kujipa jina ‘The Rolls Royce Musician From East Africa.’
 
Diamond ambaye yupo jijini Los Angeles, Marekani alikoenda kushoot video ya wimbo aliomshirikisha Ne-Yo, ameshare kipande cha video kwenye Instagram cha gari hilo na kuashiria kuwa huenda akawa amelinunua tayari.


Hata hivyo hajasema iwapo gari hilo limeshakuwa mali yake ama alikuwa tu showroom kuosha macho!
Rolls Royce, ni magari yanayozalishwa na kampuni ya Uingereza na yalianzishwa na Charles Stewart Rolls na Sir Frederick Henry Royce, March 1906. Bei yake huanzia $300,000 – $500,000.

“Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekuwa ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokuwa nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakuwa na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida,” aliiambia tovuti ya Millard Ayo miezi kadhaa iliyopita.

Alidai kuwa kwa alipofikia ni muhimu kwa na gari la hadhi yake ili kujiongezea thamani zaidi.
“Ndio maana nikipata Rolls Royce inatengeneza heshima,” alisema.