CHADEMA waahirisha Operesheni UKUTA
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kisitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike nchi nzima Septemba Mosi yaliyopewa jina la UKUTA.

Akitangaza uamuzi huo, mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa, wamefanya mazungumzo na viongozi mbalimbalia wakiwemo viongozi wa dini, BAKWATA, Baraza la Maaskofu, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Jukwaa la Katiba na Jukwaa la wahariri na kuona wana kila sababu ya kusikiliza ushauri huo.

Aidha, maandamano hayo yameahirishwa kwa mwezi mmoja ili kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka wa hali ya kisiasa nchini