Polisi avua nguo kituoni ataka arejeshwe kazini
Polisi avua nguo kituoni ataka arejeshwe kazini
Kulitokea kizaza katika kituo kimoja cha polisi nchini Kenya askari polisi aliyeacha kazi mwenyewe alipovua nguo na kusalia uchi wa mnyama akijaribu kumshinikiza inspekta mkuu jenerali wa polisi Joseph Boinnet kumrejesha kazini.

Afande huyo alivua nguo na kujifunika gunia katika kituo cha polisi cha Lang’ata jijini Nairobi mapema leo asubuhi.
Afisa huyo anadaiwa kuwa aliacha kazi mwenyewemiezi 6 iliyopita kwa madhumuni ya ''kuendeleza kazi ya bwana'' ama kuhubiri injili, hata hivyo 'kazi'' haikushika kasi ipasavyo na mara akajipata anadaiwa kope si zake.


Inspekta mkuu jenerali wa polisi wa Kenya Joseph Boinnet  Aliona kheri arejee kazini kuomba msamaha mkubwa wake lakini hilo halikumsaidia kupata unga.
Maafisa wa polisi walimkamata na kumweka rumande.


 Lakini akiwa humo alianza kuimba na kuomba kwa sauti ya juu akisema kuwa ni mwenyezi mungu tu ndiye atakayemuondoa korokoroni.
Umati wa watu ulikusanyika kutizama kihoja hicho ambacho kiliwaacha wengi waliomfahamu afande huyo katika enzi zake wasijue kilichomsibu.